IQNA

Askofu asilimu pamoja na wafuasi wake Kenya, aligeuza kanisa kuwa Msikiti

20:35 - October 15, 2017
2
Habari ID: 3471218
TEHRAN (IQNA)-Askofu wa kanisa moja nchini Kenya amesilimu pamoja na wafuasi wake kadhaa na kuligeuza kanisa lake kuwa msikiti.
Askofu asilimu pamoja na wafuasi wake Kenya, aligeuza kanisa kuwa MsikitiAliyekuwa Askofu Charles Okwany, wa kanisa ambalo lilikuwa likijulikana kama God's Call Church of East Africa amesema amesilimu baada ya kufanya utafiti wa kina kuhusu Uislamu. Aidha amesilimu pamoja na wafuasi wake kadhaa na kuligeuza kanisa lake kuwa msikiti.

Katika mahojiano na jarida la kila wiki la The Nairobian, askofu huyo wa zamani ambaye baada ya kusilimu alibadilisha jina lake na kuwa Ismail Okwany amesema moja ya sababu za kusilimu kwake ni vazi la stara la Hijabu ambalo wanawake Waislamu wanavaa na hivyo kuimarisha maadili bora. Aidha amesema akiwa mhuburi alikuwa anakerwa sana na wanawake waliokuwa wakiingia kanisani wakati wa ibada wakiwa wamevalia sketi fupi huku wakikaidi ushauri wake wa kuvaa mavazi ya heshima. Anasema wanawake wanaovaa mavazi kama hayo yasiyofaa kanisani huwa wanawachochea wahubiri kutenda dhambi.

Katika Uislamu wanawake hutakuiwa kuvaa vazi kamili la stara la Hijabu wakiwa mbele watu ajinabi na wakati wanapokuwa msikitini huswali eneo tafauti na wanaume.

"Kanisa langu ambalo lilikuwa likijulikana kama Nyalgosi God's Call Church of East Africa, na sasa litajulikana kama Nyalgosi Jamia Mosque," amesema Ismail Okwany mwenye umri wa miaka 65.

Nyalgosi ni eneo lililo katika Kaunti ya Homa Bay iliyo eneo la Nyanza magharibi mwa Kenya.

"Wakati nilipokuwa askofu, nilisafiri hadi Nairobi, Mombasa na Malindi nchini Kenya na pia katika nchi jirani ya Tanzania kuhubiri. Nilitumia fursa hiyo kujifunza kuhusu maisha na tabia za Waislamu na Wakristo katika maeneo niliyotembea na nikafikia natija kuwa, Uislamu ndio mfumo bora zaidi," amesema Okwany ambaye alisilimu Septemba 26 mwaka huu wa 2017.Askofu asilimu pamoja na wafuasi wake Kenya, aligeuza kanisa kuwa Msikiti

Anaongeza kuwa aliukmbatia Uislamu akiwa na wafuasi kadhaa wa kanisa lake ambalo sasa limegeuzwa kuwa msikiti. Anaongeza kuwa kwa ujumla kuna Waislamu 63 wanaoswali katika msikiti huo na kwamba sasa yuko mbioni kujifunza Uislamu ili aweze kuendelea na kazi yake ya kuhubiri.

Okwany anasema kumekuwa na dhana potovu katika eneo la Nyanza nchini Kenya kuwa Uislamu ni dini ya Waarabu na Wasomali tu na kwa msingi huo atajitahidi kuwaeilimisha wakazi wa eneo hilo kuwa Uislamu ni dini ya watu watu wote pasina kujali kabila.

3652764

Imechapishwa: 2
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Bila jina
0
0
Takbir,Allahu Akbar
khamis
0
0
Laailaa hailallah Muhammad Rasulullah
captcha