IQNA

Misikiti kadhaa yafungwa Saudia kuzuia maandamano dhidi ya utawala wa kifalme

19:04 - September 15, 2017
4
Habari ID: 3471175
TEHRAN (IQNA)- Misikiti kadhaa imefungwa Saudia Arabia baada ya ukoo wa kifalme kuingiwa na kiwewe kuhusu uwezekano wa kuibuka maandamano ya raia kupinga mienendo ya utawala huo.

Taarifa zinasema wanajeshi wa utawala wa Aal-Saud nchini wamevamia misikiti ya miji mbalimbali kuanzia, Qatif, Ta'if, Unaizah na Riyadh na kuifunga, kutokana na wasi wasi wake wa kuibuka maandamano ya raia kupinga mienendo ya utawala huo.

Mtandao wa habari wa al-Ahd umeripoti kwamba, kufuatia wanaharakati wa kisiasa kuwataka raia wa Saudia kufanya maandamano dhidi ya utawala wa nchi hiyo, mapema leo askari wa utawala huo walivamia misikiti kadhaa na kuwatia mbaroni maimamu wa misikiti hiyo akiwemeo Sheikh Muhammad Halawani, imamu wa msikiti wa Mfalme Fahd wa mji wa Ta'if unaopatikana katika mkoa wa Makkah, magharibi mwa Saudia na Sheikh Qatwami, imamu wa jamaa wa msikiti wa eneo la Umm Al-Hamam wa mji wa Qatif, mashariki mwa nchi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, maafisa usalama wa Saudia pia, wameipiga kufuli misikiti ya miji ya Unaizah, katikati mwa nchi, Abdullah Ibn Abbas wa mji wa Ta'if pamoja na msikiti wa Bin Nahit katika eneo la Nazim, huko Riyadh, mji mkuu wa Saudia. Kabla ya hapo baadhi ya wanaharakati wa kijamii nchini Saudia walikuwa wamewataka raia wa nchi hiyo kufanya maandamano makubwa katika maeneo tofauti kupinga udikteta wa Aal-Saud nchini humo. Wiki hii pia kulishuhudiwa wimbi la utiaji nguvuni maulamaa na wanaharakati ambao hawakuiunga mkono serikali ya Riyadh katika mgogoro wake na Bahrain lingali linaendelea kushuhudiwa nchini Saudi Arabia.Katika miaka ya hivi karibuni utwala wa Aal-Saud umekuwa ukitumia mkono wa chuma kujaribu kuzima malalamiko ya wapinzani, ambapo katika harakati hiyo makumi ya raia wametiwa nguvuni na wengine wengi kuhukumiwa adhabu ya kifo.


3642072

Imechapishwa: 4
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Ismail iasa
0
0
Wafalme wasaudia wengi sio waarabu ,wengiwao wayahudi kwahyo lazma wawe naroho mbaya
muhammad shkely
0
0
Lsaudi wasililizeni raia wanahitaji nini
Bila jina
0
0
maasaud wanahofia kuanguka kwa falme zao.
MOHAMED
0
0
MFALME HIZO ZITAANGUKA INSHALLAH.ZIMEDHULUMU UMMA SIKU NYINGI NA KUIFANYA HIJJAZ NI MALI YAO.
captcha