IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Vijana wasomi Wairani wanapaswa kuimarisha wigo wa elimu na teknolojia

9:08 - August 08, 2019
Habari ID: 3472074
TEHRAN (IQNA) -Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: "Ustawi wa sayansi zenye faida kwa Iran ni jambo linalowezekana na ustawi huo unapaswa kuwa kwa msingi mtazamo wa kimapinduzi na fikra za Kiislamu."

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei ameyasema hayo leo Jumatano mjini Tehran wakati alipokutana na vijana kadhaa wasomi bingwa wenye vipaji ambao wamepata medali katika Olimpiadi za kimataifa za sayansi na pia vijana wa timu ya taifa ya voliboli ya Iran ambao wamefika katika kilele cha mchezo huo duniani. Katika kikao hicho, Kiongozi Muadhamu amesema vijana wasomi bingwa Wairani wanapaswa kuhakikisha kuwa wanapanua zaidi mipaka ya ustawi wa elimu na teknolojia.

Kiongozi Muadhamu amewapongeza  vijana hao kutokana na uhodari, umahiri na busara yao na kusistiza kuwa, njia hiyo ya utaalamu bingwa haipaswi kuwa na kikomo.

Ayatullah Khamenei pia ameashiria namna ambayo katika karne mbili zilizopita taifa la Iran lilivyokuwa limelazimishwa kubakia nyuma hasa katika zama za Wafalme wa Kiqajari na Kipahlavi na kusema: "Baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na hasa miaka 20 iliyopita, kumekuwa na jitihada kubwa za ustawi wa sayansi na teknolojia lakini bado tuko nyuma na hivyo ni jukumu la vijana wasomi bingwa wenye vipaji kuchukua hatua za kuimarisha kasi ya mafanikio katika nyuga za sayansi na teknolojia."

Kiongozi Muadhamu pia ameashiria namna Iran imeweza kupata nafasi za juu duniani katika uga wa teknolojia ya nano na kusema sasa inatazamiwa kuwa vijana wasomi bingwa wenye vipaji na kizazi kijacho wataweza kupata mafanikio zaidi katika uga huu na wasitosheke na waliyoweza kupata.

Ayatullah Khamenei amewashukuru vijana wasomi bingwa waliopata medali za kimataifa kutokana na hatua yao ya kumtunuku medali hizo na kusema medali hizo hajakabidhiwa yeye kama mtu binafsi bali kitendo hicho ni nembo tu ya heshima. Amesema hata baada ya kukubali kutunukiwa medali hizo kutoka kwa vijana hao azizi na wasomi bingwa, atawarejeshea ili wabaki nazo.

http://iqna.ir/fa/news/3833247

captcha